Local,Normal News,Ligi Kuu, Yanga, Fountain, JKT, Pamba, Mtibwa, Prisons

Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18 Jun 2026
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo

Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mechi tatu za kuhitimisha raundi ya 27 zinatarajiwa kupigwa.

Mabingwa watetezi Yanga watakuwa na shughuli pevu mbele ya Fountain Gate katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Ili kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi Yanga inahitaji ushindi au hata matokeo ya sare. Hata hivyo sare inaweza kuwaongezea presha zaidi kufikia malengo yao ya kutetea ubingwa hasa kwa kuzingatia watakuwa na mechi nyingine tatu ngumu dhidi ya Azam Fc, TRA United na JKT Tanzania.

Ushindi wa bao 1-0 ambao watani zao Simba waliupata dhidi ya Mbeya City umewaweka kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama moja baada y kufikisha alama 64.

Hata hivyo Wananchi wasitarajie mtaremko kutoka kwa Fountain Gate kwani nao wanazihitaji alama tatu ili kujiondoa kwenye presha ya kucheza play-off au kushuka daraja.

Pamba Jiji itachuana na Mtibwa Sugar katika mchezo mwingine utakaopigwa saa 10 jioni huku JKT Tanzania wakiikaribisha Tanzania Prisons katika mtanange ambao pia utapigwa saa 10.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
23h ago
READ MORE β†’