Local,Transfer News,Azam Fc

Himid aongeza mwaka Azam Fc

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Jun 2026
Himid aongeza mwaka Azam Fc

Klabu ya Azam FC imethibitisha rasmi kumuongezea mkataba kiungo wake mkongwe, Hemed Mao Mkami, ambaye ataendelea kubaki katika kikosi hicho hadi mwaka 2027.

Nyota huyo amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja ambao unaongeza muda wake wa kuitumikia klabu hiyo ya Chamazi, hatua inayoonesha imani kubwa ya benchi la ufundi na uongozi wa Azam FC kwa mchango wake ndani ya timu.

Himed Mao alirejea Azam FC msimu uliopita baada ya takribani misimu sita ya kucheza soka la kulipwa nchini Misri, ambako alijipatia uzoefu mkubwa katika mazingira ya ushindani wa juu. Uzoefu huo umeendelea kumfanya kuwa miongoni mwa wachezaji muhimu zaidi katika safu ya kiungo ya Azam FC.

Tangu kurejea kwake, Mao amekuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa timu, akicheza nafasi ya kiungo wa kati kwa nidhamu, uimara na uwezo wa kuongoza mchezo. Uwepo wake umeongeza uthabiti katika eneo la kiungo.

Hatua ya klabu hiyo kuongeza mkataba wa Himed Mao inaonesha dhamira ya Azam FC ya kubaki na msingi imara wa wachezaji wenye uzoefu, huku ikiendelea kujenga kikosi chenye mchanganyiko wa vijana na wazoefu.

More Stories

Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
2h ago
READ MORE β†’
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
6h ago
READ MORE β†’
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
7h ago
READ MORE β†’
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
9h ago
READ MORE β†’
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
9h ago
READ MORE β†’
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
13h ago
READ MORE β†’
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
15h ago
READ MORE β†’
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
15h ago
READ MORE β†’
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
1d ago
READ MORE β†’
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
1d ago
READ MORE β†’