Local,Normal News,Yanga

Pacome afunguka changamoto ya majeraha, atoa ahadi kwa Wananchi

Joel JJ By Joel JJ
19 Jun 2026
Pacome afunguka changamoto ya majeraha, atoa ahadi kwa Wananchi

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua, ameweka wazi kuwa amekumbana na changamoto kubwa ya majeraha msimu huu, hali iliyomlazimu kucheza baadhi ya mechi akiwa na maumivu makali ya goti.

Nyota huyo, anayejulikana kwa uwezo wake mkubwa wa kutengeneza na kufunga mabao, amesema kipindi hicho kilikuwa kigumu kwake, lakini sasa ameimarika na yuko tayari kuisaidia Yanga katika mechi zilizosalia kabla ya kufungwa kwa msimu.

Pacome alionyesha kurejea katika kiwango chake bora baada ya kufunga bao la kwanza la Yanga kwenye ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate. Bao hilo lilikuwa muhimu kwake binafsi na kwa timu katika harakati za kutimiza malengo ya msimu.

Baada ya kufunga, Pacome alionyesha ishara maalumu ya shukrani kuelekea kwa mashabiki wa Yanga, akieleza kuwa ilikuwa ni njia yake ya kuwashukuru kwa sapoti waliompa katika kipindi chote alichokuwa akipambana na majeraha.

“Ishara ile ni kuwashukuru mashabiki wa Yanga ambao wameweza kunivumilia katika kipindi kigumu. Nilicheza nikiwa na maumivu kwenye goti kwa kipindi kirefu kidogo lakini mara zote wamekuwa pamoja na mimi hata ninapokuwa katika nyakati ngumu uwanjani,” alisema Pacome.

Aliongeza kuwa bao alilofunga dhidi ya Fountain Gate lina maana kubwa kwake katika hatua hii muhimu ya mwisho wa msimu.

“Goli dhidi ya Fountain Gate ni muhimu sana kwangu katika wakati huu tunapoelekea mwisho wa msimu. Najiskia vizuri sasa na niko tayari kuwapa mashabiki wetu kile wanachokitarajia kutoka kwetu. Waje kwa wingi uwanjani kutusapoti kwenye mechi hizi za mwisho,” aliongeza.

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
15h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
16h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
18h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
18h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
19h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
19h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
20h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
20h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
20h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
22h ago
READ MORE →