Local,Normal News,CRDB Cup, Yanga, Azam

Makocha Yanga, Azam FC watambiana kuelekea nusu fainali Kombe la CRDB

Joel JJ By Joel JJ
20 Jun 2026
Makocha Yanga, Azam FC watambiana kuelekea nusu fainali Kombe la CRDB

Makocha wa Yanga na Azam FC wameonyesha kujiamini huku wakitambiana kuelekea mchezo wa nusu fainali ya Kombe la CRDB unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Kocha wa Yanga, Abdihamid Moalin, amesema ni heshima kubwa kwa klabu hiyo kufanikiwa kucheza hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo, huku akisisitiza kuwa lengo lao kuu ni kushinda mchezo huo na kutinga fainali.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo, Moalin aliwapongeza wachezaji wake kwa kuendelea kuonyesha kiu ya mafanikio na ushindani wa hali ya juu katika mashindano mbalimbali.

“Tumewasili salama na maandalizi ya mchezo wa kesho yanaendelea vizuri. Wachezaji wako katika hali nzuri kiakili na kimwili na tunafahamu kile kinachohitajika kufanyika,” alisema Moalin.

Aliongeza kuwa uzoefu wa kikosi chake katika mechi kubwa ni moja ya silaha muhimu itakayowasaidia katika pambano hilo.

“Ni heshima kubwa kucheza nusu fainali ya mashindano kama haya. Tumestahili kufika hapa lakini lengo letu ni kufika fainali. Ili kufanya hivyo, tunapaswa kuwa bora katika wakati huu na kushinda kesho,” alisema.

Moalin pia aliwataka wachezaji wake kuendelea kuwa wanyenyekevu na wenye njaa ya ushindi licha ya mafanikio waliyoyapata katika misimu iliyopita.

“Tunapaswa kubaki wanyenyekevu, wenye njaa ya mafanikio na tusichoke kushinda. Kushinda ni jambo la kipekee ambalo timu nyingi zinatamani kulifikia. Huu ni mwaka mwingine na fursa nyingine ya kuandika historia mpya,” alisisitiza.

Aidha, aliwaomba mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao katika mchezo huo muhimu.

Kwa upande wa Azam FC, Kocha Mkuu Florent Ibenge amesema anatambua ugumu wa kukabiliana na Yanga, lakini amesisitiza kuwa kikosi chake kimejiandaa vya kutosha kuhakikisha kinapata ushindi na kufuzu hatua ya fainali.

“Tunajua ni mchezo mgumu dhidi ya Yanga lakini sisi tumejiandaa kimbinu kuweza kushinda. Tumecheza nao mara tatu, mechi moja tumetoka sare na tumepoteza mechi mbili, moja ikiwa kwa mikwaju ya penalti. Matokeo haya yanaonyesha hatuko mbali nao,” alisema Ibenge.

Kocha huyo raia wa DR Congo aliongeza kuwa licha ya Yanga kuonekana kuwa na nafasi kubwa kutokana na ubora wao wa hivi karibuni, Azam FC itaingia uwanjani ikiwa na lengo moja tu la kuibuka na ushindi.

“Najua wao watakuwa juu kwenye mchezo huo lakini sisi tutakuwa tayari na tunataka kushinda ili tuweze kufuzu fainali,” alisema.

Mchezo huo wa nusu fainali ya Kombe la CRDB utapigwa kesho Jumapili Juni 21 katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

More Stories

Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
1h ago
READ MORE →
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
5h ago
READ MORE →
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
6h ago
READ MORE →
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
8h ago
READ MORE →
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
8h ago
READ MORE →
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
12h ago
READ MORE →
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
14h ago
READ MORE →
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
15h ago
READ MORE →
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
1d ago
READ MORE →
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
1d ago
READ MORE →