Algeria imejiweka katika nafasi nzuri ya kuwania tiketi ya hatua inayofuata ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Jordan katika mchezo wa Kundi J uliochezwa kwenye Uwanja wa Levi's Stadium, Santa Clara. Ushindi huo umerejesha matumaini ya Les Fennecs kufuzu hatua ya 32 bora baada ya kuanza mashindano kwa matokeo yasiyoridhisha dhidi ya Argentina.





