Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza tarehe ya mchezo wa fainali kombe la CRDB kati ya Simba dhidi ya Azam Fc.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF mapema leo, mchezo huo sasa utapigwa Julai 04 kwenye uwanja wa Gombani, Pemba visiwani Zanzibar.
Simba na Azam Fc zilitinga fainali baada ya kushinda mechi zao za nusu fainali. Simba iliichapa Coastal Union mabao 4-0 wakati Azam Fc ikiichapa Yanga mabao 3-2




