Kocha wa zamani wa Yanga, Romain Folz, amepata changamoto mpya baada ya kuteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa US Monastir ya Tunisia kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Folz, raia wa Ufaransa mwenye uzoefu mkubwa katika soka la Afrika, amerejea tena kwenye majukumu ya ukocha mkuu baada ya kusubiri kwa miezi kadhaa tangu alipoachana na Yanga mwanzoni mwa msimu huu.





