Kiungo mkongwe Mzamiru Yassin amejiunga rasmi na TRA United kwa mkataba wa miaka miwili akitua kama mchezaji huru kufuatia kumalizika kwa mkataba wake na Simba.
Mzamiru anarejea TRA United baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa mkopo wa msimu mzima wa 2025/26, ambapo alionyesha kiwango cha kuvutia na kuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika kikosi cha kocha Etiene Ndayiragije.





