International,Transfer News,Barcelona, Dortmund

Adeyemi ni suala la muda Barcelona

Joel JJ By Joel JJ
β€’
9 Jul 2026
Adeyemi ni suala la muda Barcelona

Fc Barcelona imepiga hatua kubwa katika harakati za kumsajili kiungo mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Karim Adeyemi, baada ya kufikia makubaliano binafsi na mchezaji huyo, huku mazungumzo kati ya klabu hizo mbili kuhusu ada ya uhamisho yakiendelea.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa waandishi nguli wa masuala ya usajili Fabrizio Romano na Gerardo Romero, Adeyemi ameonyesha wazi kuwa anataka kujiunga na Barcelona pekee katika dirisha hili la usajili. Inadaiwa tayari amekubaliana masharti ya mkataba binafsi na miamba hiyo ya La Liga, hatua inayoiweka Barcelona katika nafasi nzuri ya kukamilisha dili hilo.

Ripoti zinaeleza kuwa Barcelona tayari imewasilisha ofa rasmi kwa Borussia Dortmund, huku viongozi wa klabu hiyo ya Ujerumani wakifanya tathmini ya ofa hiyo kabla ya kutoa uamuzi. Mazungumzo yanaendelea kuhusu kiasi cha ada ya usajili, kwani Adeyemi bado ana mkataba unaomfunga Dortmund hadi mwaka 2027.

Kocha Hansi Flick anatajwa kuwa mmoja wa watu waliomsukuma zaidi Adeyemi kutua Camp Nou. Inaelezwa kuwa Flick amezungumza binafsi na nyota huyo wa Ujerumani kuhusu nafasi yake ndani ya kikosi na mradi wa Barcelona wa msimu ujao, jambo lililochangia mchezaji huyo kukubali kuhamia Catalunya.

Adeyemi, mwenye umri wa miaka 24, anasifika kwa kasi yake, uwezo wa kucheza pande zote mbili za winga pamoja na nafasi ya mshambuliaji wa kati. Barcelona inaamini kuwa atakuwa nyongeza muhimu katika safu ya ushambuliaji kuelekea msimu mpya.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’