Local,Normal News,Ligi Kuu, Yanga, Singida

Mossi, Moalin wasepa na tuzo za ligi kuu Juni 2026

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Jul 2026
Mossi, Moalin wasepa na tuzo za ligi kuu Juni 2026

Kiungo mshambuliaiiji wa Singida Black Stars, Ndumumwe Mossi amechaguliwa kuwa mchezaji Bora wa mwezi Juni wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2025/26, huku Abdihamid Moalin wa Young Africans akichaguliwa Kocha Bora wa ligi hiyo kwa mwezi huo.

Mossi na Moalin wametwaa tuzo hizo baada ya uchambuzi uliofanywa na kikao cha Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jumatatu Julai 6, 2026.

Mossi alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo kwa mwezi huo ikiwa ni pamoja na kufunga mabao nane zikiwemo 'hat-trick' mbili katika dakika 440 za michezo mitano ambayo Singida ilicheza mwezi huo, akiwashinda Maxi Nzengeli wa Young Africans na Elie Mpanzu wa Simba alioingia nao fainali.

Kwa upande wa Moalin aliyeingia fainali na Steve Barker wa Simba na Florent Ibenge wa Azam, aliiongoza timu yake kushinda michezo yote mitano iliyocheza mwezi huo.

Pia Kamati ya Tuzo za TFF ilimchagua Frank Ikobela wa Transit Camp kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Juni wa Ligi ya Championship ya NBC, huku Zuberi Katwila wa Geita Gold akichaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Juni kwenye ligi hiyo.

Ikobela aliwashinda Rishedy Kihedu wa Mbuni na Maulid Shabani wa Geita Gold alioingia nao fainali, wakati Katwila aliwashinda Juma Kaseja wa Kagera Sugar na Mbwana Makata wa Polisi Tanzania.

Pia Meneja wa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Said Mpuche amechaguliwa kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Juni kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

Aidha Kamati imeteua mabao matatu ambayo yatapigiwa kura na mashabiki ili kupata bao bora la mwezi Juni, mabao hayo na michezo katika mabano ni Hassan Kabunda dakika ya tano (Namungo v Mbeya City), Eliud Ambokile dakika ya 28 (Namungo na Mbeya City) na Juma Luizior dakika ya 85 (Prisons v Mtibwa Sugar).

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
23h ago
READ MORE β†’