inaendelea na mchakato wa kukiimarisha kikosi chake kuelekea msimu wa 2026/27, huku moja ya maeneo yanayopewa kipaumbele ikiwa ni kuongeza idadi ya wachezaji wazawa kulingana na mahitaji ya usajili.
Taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa klabu hiyo wako kwenye mazungumzo na kiungo wa Taifa Stars, Alphonce Mabula Msanga, wakilenga kumrejesha nchini baada ya kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania kwa miaka kadhaa.
Yanga inavutiwa na uwezo wa Mabula wa kucheza nafasi ya kiungo mkabaji, huku ikiamini uzoefu wake wa kimataifa unaweza kuongeza ushindani na uimara katika safu ya kiungo. Inaelezwa kuwa Mabula kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Shamakhi FK ya Azerbaijan.
Fursa hiyo imeifanya Yanga kuharakisha mazungumzo, hasa ikizingatiwa kuwa kiungo huyo yupo nchini kwa mapumziko ya mwisho wa msimu. Ingawa hakuna taarifa rasmi kutoka pande zote mbili, mazungumzo yanaendelea na inaelezwa kuwa Yanga imewasilisha ofa yenye lengo la kumshawishi nyota huyo kuvaa jezi ya mabingwa hao wa Ligi Kuu ya NBC katika msimu ujao.