Local,Transfer News,Yanga Sc, Singida BS

Yanga yakaribia kumnasa Chukwu kutoka Singida BS

Joel JJ By Joel JJ
β€’
20 Jul 2026
Yanga yakaribia kumnasa Chukwu kutoka Singida BS

Klabu ya Yanga SC imeendelea kufanya maboresho makubwa kwenye kikosi chake kwa lengo la kuendelea kutawala soka la Tanzania baada ya misimu mitano mfululizo ya mafanikio.

Miongoni mwa maeneo ambayo mabingwa hao wameonekana kulipa kipaumbele ni nafasi ya kiungo mkabaji, ambapo taarifa zinaeleza kuwa mchakato wa kumnasa nyota wa Nigeria, Morrice Chukwu, umefikia hatua za mwisho.

Chukwu kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Singida Black Stars. Klabu hiyo kutoka mkoani Singida ilikuwa kwenye mipango ya kumuongezea mkataba mpya, lakini mazungumzo hayo yanadaiwa kuvurugika baada ya Yanga kuingia kwenye mbio za kuwania saini yake.

Ikiwa mambo yataenda kama yanavyopangwa, Chukwu anatarajiwa kujiunga na Yanga SC na kuimarisha safu ya kiungo ya timu hiyo. Hatua hiyo inakuja wakati Singida BS ikimpokea tena Mohamed Damaro ambaye amerejea baada ya kumalizika kwa muda wake wa mkopo wa miezi sita.

Chukwu amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Singida BS kwa misimu miwili iliyopita, akionyesha uwezo mkubwa katika nafasi ya kiungo mkabaji pamoja na kucheza kama beki wa kati pale inapohitajika.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’