Simba SC imemtambulisha rasmi winga Bakari Msimu kuwa mchezaji mpya wa klabu hiyo kuelekea msimu wa 2026/27, akitokea Coastal Union.
Bakari Msimu anajiunga na Wekundu wa Msimbazi baada ya kuonyesha kiwango kizuri akiwa Coastal Union, ambapo alivutia kwa kasi, uwezo wa kupiga chenga na kutengeneza nafasi za mabao.
Usajili wake unaongeza ushindani katika safu ya ushambuliaji ya Simba, huku benchi la ufundi likiamini atatoa mchango mkubwa katika harakati za kutwaa mataji ya ndani na kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa msimu ujao.