Young Africans SC wameachana rasmi na kiungo wa kati Lassine Kouma (22), hivyo kumaliza ushirikiano wao kuelekea maandalizi ya msimu wa 2026/27.
Nyota huyo mwenye uraia wa Mali/Chad sasa ni mchezaji huru na tayari ameanza kutafuta klabu mpya kwa ajili ya kuendelea na maisha yake ya soka baada ya kuondoka Jangwani.
Kuondoka kwa Kouma ni sehemu ya mabadiliko yanayoendelea ndani ya kikosi cha Yanga, huku uongozi wa klabu ukiendelea kufanya maboresho ya kikosi kwa kuwasajili wachezaji wapya na kuachana na baadhi ya waliokuwepo.
Katika dirisha hili la usajili, Yanga imekuwa miongoni mwa klabu zenye shughuli nyingi, ikiongeza nyota wapya katika kikosi huku ikijiandaa kutetea mataji ya ndani na kufanya vizuri zaidi kwenye michuano ya CAF.