Simba SC inamaliza mashindano kwenye michuano ya CECAFA Kagame Cup 2026 kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Amahoro, Kigali, Rwanda.
Licha ya kuonyesha kiwango kizuri na kuondoka na alama tatu, ushindi huo haukutosha kuipa Simba nafasi ya kusonga mbele kwenye hatua inayofuata ya mashindano.





