Klabu ya Simba SC leo imefanikisha zoezi la uchangiaji damu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Simba, kwa kushirikiana na Taasisi ya Mo Dewji. Zoezi hilo limefanyika katika vituo vya Karume na Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, ambapo Wanasimba na wananchi mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kushiriki kuchangia damu kwa ajili ya kusaidia wenye uhitaji.





