Fulham wamekamilisha rasmi usajili wa mshambuliaji wa Hispania, Gonzalo García, kutoka Real Madrid kwa ada inayoripotiwa kufikia Pauni milioni 34.
Nyota huyo ametambulishwa rasmi leo na klabu hiyo ya Ligi Kuu England baada ya kukamilisha taratibu zote za uhamisho, akianza rasmi sura mpya ya maisha yake ya soka katika dimba la Craven Cottage.





