Klabu ya RS Berkane ya Morocco imemtambulisha rasmi kocha wa Ureno mwenye asili ya Cape Verde, Pedro Leitão Brito, maarufu kama Bubista, kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili utakaodumu hadi mwaka 2028. Bubista anachukua nafasi iliyoachwa na Moine Chaâbani, ambaye ameondoka klabuni hapo na kwenda kuiongoza Timu ya Taifa ya Tunisia.





