Arsenal wamekamilisha rasmi makubaliano ya kumsajili kiungo wa kimataifa wa Brazil, Bruno Guimarães, kutoka Newcastle United katika moja ya usajili mkubwa wa dirisha hili la usajili.
Kwa mujibu wa Fabrizio Romano, makubaliano kati ya Arsenal na Newcastle yamefikiwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu, huku ada ya uhamisho ikitajwa kufikia Pauni milioni 75 (£75m).





