Wakati akitambulisha kikosi cha Yanga kuelekea msimu wa mashindano 2026/27, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alitangaza taarifa za kuwaongeza baadhi ya nyota wa timu hiyo mikataba.
Nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto, mlinda lango Djigui Diarra, Yao Kouassi na Ibrahim Bacca wote wameongeza mikataba yao ya kuendelea kusalia jangwani kwa miaka mingine miwili.





