Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina, Julian Alvarez, amerejea jijini Madrid leo Jumatatu, Agosti 10, 2026, kufuatia mapumziko mafupi baada ya fainali za Kombe la Dunia.
Nyota huyo aliwasili asubuhi na mapema na kuelekea moja kwa moja katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Vithas Madrid Arturo Soria kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya (medical tests).





