Kocha Mkuu wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi, amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC utakaochezwa kesho, Agosti 12. Mngqithi amesema Yanga imefanya maandalizi ya kutosha katika kipindi cha pre-season na anaamini timu yake iko katika ubora wa kutosha kupata ushindi katika mchezo huo wa ufunguzi wa msimu wa 2026/27.





