Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi simba Crescentius Magoli amesema kuwa tayari timu hiyo ilikamilisha usajili wa Selemani Mwalimu wa mkopo kabla ya upande wa mchezaji kubadili mtazamo na makubaliano na Simba.
Magoli amesema hayo hii leo baada ya kuwasili visiwani zanzibar ambako siku ya kesho Wekundu wa msimbazi simba watakutana na watani zao Yanga.





