Kiungo wa Yanga SC, Allan Okello, huenda asionekane kwenye kikosi cha timu hiyo msimu huu baada ya Wydad AC kuwasilisha ofa ya kutaka kumsajili.
Okello amekuwa miongoni mwa wachezaji wenye uwezo wa kutengeneza nafasi, kucheza mipira ya mwisho na kuongeza ubunifu katika eneo la kiungo, hivyo kuondoka kwake kunaweza kuacha pengo kwenye kikosi cha Yanga.





