Kiungo wa Azam FC na Timu ya Taifa ya Tanzania, Feisal Salum “Fei Toto”, anatarajiwa kukutana na viongozi wa juu wa klabu hiyo kesho Jumatano kwa ajili ya majadiliano kuhusu mkataba mpya.
Kikao hicho awali kilipangwa kufanyika Jumatatu, lakini kimeahirishwa hadi kesho, huku viongozi wakuu wa Azam FC wakitarajiwa kuhudhuria mazungumzo hayo.





