Mshambuliaji wa pembeni wa Afrika Kusini, Thapelo Maseko, ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa FC Copenhagen ya Denmark baada ya kukamilisha uhamisho wake kutoka Mamelodi Sundowns.
Maseko anaondoka Sundowns baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa misimu kadhaa, huku Mamelodi Sundowns ikimuaga rasmi na kumtakia kila la heri katika hatua yake mpya ya soka barani Ulaya.





