Serikali: Tamasha la Taifa kuchochea utamaduni, utaifa na uchumi bunifu

Jairo Mtitu By Jairo Mtitu
β€’
24 Aug 2026
Serikali: Tamasha la Taifa kuchochea utamaduni, utaifa na uchumi bunifu

Serikali imesema Tamasha la Taifa litakuwa nyenzo muhimu katika kulinda, kutunza na kuendeleza utamaduni wa Mtanzania, huku likitumika pia kuimarisha utaifa na mshikamano, kukuza uchumi bunifu, kufungua fursa za ajira na biashara, pamoja na kuitangaza Tanzania kupitia utalii wa kiutamaduni.

Akitoa taarifa kuhusu maandalizi ya tamasha hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema tamasha hilo linatarajiwa kufanyika mkoani Morogoro kuanzia Agosti 25 hadi 29, 2026.

Msigwa amesema tamasha hilo litawakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya utamaduni na ubunifu, likiwemo vikundi 28 vya utamaduni, wasanii 30, wajasiriamali 70 pamoja na vijana 5,000.

Amesema uwepo wa makundi hayo unalenga kutoa nafasi kwa washiriki kuonyesha vipaji, bidhaa na kazi zao za ubunifu, huku wananchi wakipata fursa ya kujifunza na kufurahia utajiri wa tamaduni mbalimbali zinazopatikana nchini.

Kwa mujibu wa Msigwa, tamasha hilo pia ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha utamaduni wa Tanzania unatambulika zaidi ndani na nje ya nchi, sambamba na kutumia utamaduni kama chanzo cha fursa za kiuchumi, ajira na biashara kwa wananchi, hasa vijana.

Aidha, ametoa rai kwa wananchi kushiriki kwa wingi katika Tamasha la Taifa ili kupata nafasi ya kushuhudia na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na utamaduni wa Mtanzania, ikiwemo ngoma za asili, vyakula vya asili na mavazi ya asili.

Mbali na burudani na maonesho ya kitamaduni, tamasha hilo pia litakuwa na mdahalo wa kitaifa utakaojikita katika kuwawezesha vijana kushiriki katika kulinda maadili, hatua ambayo Serikali inaamini itasaidia kujenga kizazi kinachothamini utamaduni na misingi ya maadili ya taifa.

Serikali imeendelea kusisitiza umuhimu wa utamaduni katika kujenga umoja wa kitaifa na kukuza uchumi, huku Tamasha la Taifa likitarajiwa kuwa moja ya majukwaa yatakayounganisha utamaduni, ubunifu, biashara na utalii kwa manufaa ya Watanzania.

ADVERTISE HERE

More Stories

JKT Tanzania, Fountain Gate watamba kuelekea mtanange wa NBC Premier League
JKT Tanzania, Fountain Gate watamba kuelekea mtanange wa NBC Premier League
49m ago
READ MORE β†’
TPLB yaweka msisitizo wa wajibu kabla ya Kariakoo Derby
TPLB yaweka msisitizo wa wajibu kabla ya Kariakoo Derby
1h ago
READ MORE β†’
Kariakoo Derby - mfumo wa tiketi warejea utaratibu wa awali
Kariakoo Derby - mfumo wa tiketi warejea utaratibu wa awali
1h ago
READ MORE β†’
Ronaldo amtumia Messi ujumbe wa heshima baada ya kuaga Argentina
Ronaldo amtumia Messi ujumbe wa heshima baada ya kuaga Argentina
2h ago
READ MORE β†’
Ligi Kuu NBC inaendelea leo Alhamisi baada ya FIFA break
Ligi Kuu NBC inaendelea leo Alhamisi baada ya FIFA break
2h ago
READ MORE β†’
Wanasimba wajivunia Libasse Gueye kuelekea mtanange wa dabi dhidi ya Yanga
Wanasimba wajivunia Libasse Gueye kuelekea mtanange wa dabi dhidi ya Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Taifa stars yashuka nafasi tatu viwango vya fifa
Taifa stars yashuka nafasi tatu viwango vya fifa
2h ago
READ MORE β†’
Simba yataja sababu kuchelewa mauzo ya tiketi
Simba yataja sababu kuchelewa mauzo ya tiketi
5h ago
READ MORE β†’
Msimu wa tatu wa Safari Lager Cup wazinduliwa
Msimu wa tatu wa Safari Lager Cup wazinduliwa
20h ago
READ MORE β†’
Pedro astaafu soka baada ya safari yenye mafanikio.
Pedro astaafu soka baada ya safari yenye mafanikio.
22h ago
READ MORE β†’