Nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa msimu wa 2025/26, ikiwa ni mara yake ya kwanza kushinda tuzo hiyo tangu aanze kucheza soka la ushindani.
Fernandes alikuwa na msimu bora huku akivunja rekodi ya asisti nyingi zaidi katika msimu mmoja wa Ligi Kuu England baada ya kufikisha jumla ya asisti 21, akipita rekodi zilizokuwa zikishikiliwa na Thierry Henry na Kevin De Bruyne.
Mbali na asisti hizo, kiungo huyo wa Ureno alifunga mabao tisa na kuwa miongoni mwa wachezaji muhimu katika kuisaidia Manchester United kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England chini ya kocha Michael Carrick, hivyo kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu unaofuata.



