Jonathan Sowah afunguka kuhusu tukio la kuchana picha ya Raisi wa Yanga.

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media • 3rd September 2026

Jonathan Sowah afunguka kuhusu tukio la kuchana picha ya Raisi wa Yanga.

Mshambuliaji wa Ghana, Jonathan Sowah, amezungumzia tukio lililowahi kuibua mjadala mkubwa wakati akitambulishwa kama mchezaji wa Simba SC, ambapo alionekana kuchana picha ya Rais wa Yanga SC, Eng. Hersi Said.

Sowah amesema kitendo hicho hakikuwa uamuzi wake binafsi, akieleza kuwa wakati huo hakuwa na namna wala chaguo la kufanya tofauti na alichoelekezwa. Kwa mujibu wa mshambuliaji huyo, alikuja Tanzania akiwa na lengo la kutafuta maisha na kipato kupitia soka.

“Kuna wakati huwa najisikia vibaya, kile kilichotokea sikuwa na namna wala sikuwa na chaguo lolote. Nilikuja huku kutafuta pesa, nilipaswa kufanya kile wanachotaka nifanye.”

Kauli hiyo imefungua mjadala mpya kuhusu tukio hilo, huku Sowah akisisitiza kuwa hakuchukua hatua hiyo kwa hiari yake. Tukio hilo lilitokea katika mazingira ya utambulisho wake Simba na baadaye likawa miongoni mwa matukio yaliyokumbukwa na mashabiki wa soka nchini.

Kwa sasa Sowah anaendelea na safari yake ya soka akiwa na Singida Black Stars, baada ya kuondoka Simba SC, huku akitazamia kuacha matukio ya nje ya uwanja na kuendelea kujenga jina lake kupitia uwezo wake ndani ya uwanja.

More Stories

Jonathan Sowah afunguka kuhusu tukio la kuchana picha ya Raisi wa Yanga.
Jonathan Sowah afunguka kuhusu tukio la kuchana picha ya Raisi wa Yanga.
Today, READ MORE →
TPLB yasisitiza, mabadiliko ya ratiba hayataathiri mwisho wa ligi
TPLB yasisitiza, mabadiliko ya ratiba hayataathiri mwisho wa ligi
Today, READ MORE →
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 03 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 03 2026
Today, READ MORE →
Al Ahli Tripoli yawasili Zanzibar kwa mtanange wa CAF dhidi ya KMKM.
Al Ahli Tripoli yawasili Zanzibar kwa mtanange wa CAF dhidi ya KMKM.
Today, READ MORE →
Gaborone United Yaitambua Yanga: “Hautakuwa Mchezo Mwepesi”
Gaborone United Yaitambua Yanga: “Hautakuwa Mchezo Mwepesi”
Today, READ MORE →
Kwa Shalulile Simba walianza Yanga wakamaliza, kocha Barker akihusika
Kwa Shalulile Simba walianza Yanga wakamaliza, kocha Barker akihusika
Today, READ MORE →
Yanga kumtumia Fabrizio romano kutambulisha jezi si jambo jipya
Yanga kumtumia Fabrizio romano kutambulisha jezi si jambo jipya
Today, READ MORE →
Fabrizio Romano Azindua Jezi za Yanga kwa Ajili ya CAF Champions League.
Fabrizio Romano Azindua Jezi za Yanga kwa Ajili ya CAF Champions League.
Today, READ MORE →
Simba yatangaza ujio wa Simba marathon kwenye maadhimisho ya miaka 90
Simba yatangaza ujio wa Simba marathon kwenye maadhimisho ya miaka 90
Yesterday, READ MORE →
Uganda U23 yajitoa kwenye mbio za kufuzu AFCON U23 2027
Uganda U23 yajitoa kwenye mbio za kufuzu AFCON U23 2027
Yesterday, READ MORE →