Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, ametoa ujumbe kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mighty Wanderers ya Malawi, huku akiwataka mashabiki kuendelea kuisapoti timu hiyo katika safari yake ya kimataifa.
Ahmed ametoa kauli hiyo wakati mashabiki wa Simba wakianza safari kwa magari kuelekea Malawi kwa ajili ya kuungana na timu na kutoa sapoti katika mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba itashuka uwanjani Jumapili dhidi ya Mighty Wanderers, katika mchezo utakaochezwa nchini Malawi majira ya saa 10:00 jioni, huku Wekundu wa Msimbazi wakilenga kuanza kampeni zao za kimataifa kwa matokeo mazuri.



