Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama, amefunguka kuhusu ugumu alioupitia wakati akicheza dhidi ya Simba akiwa amevaa jezi ya timu nyingine, akieleza kuwa ilikuwa changamoto kutokana na uhusiano wake mkubwa na klabu hiyo.
Chama amesema kucheza dhidi ya timu ambayo ipo moyoni mwake haikuwa rahisi, lakini alilazimika kuweka hisia pembeni na kutekeleza majukumu yake ya kikazi kwa kiwango cha juu. “Ni ngumu sana kucheza dhidi ya timu ambayo ipo kwenye moyo wako, lakini linapokuja suala la professionalism lazima ujitoe kwa uwezo wako wote,” amesema Chama.
Chama, ambaye amewahi kuichezea Yanga SC na Singida Black Stars baada ya kuondoka Simba, hatimaye amerejea Msimbazi na kwa sasa anaendelea kuitumikia Simba katika msimu huu.



