Local, Normal News, Azam Fc

Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5h ago
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20

Klabu ya Azam FC imepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha kipa wake wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 (U-20), Iddy Salim, aliyefariki dunia baada ya kupata ajali ya bodaboda.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Azam FC leo, Ijumaa, Septemba 11, 2026, Iddy Salim amefariki dunia jana, Alhamisi, Septemba 10, 2026, kufuatia ajali hiyo ya pikipiki.

“Tunasikitika kutangaza kifo cha kipa wetu wa timu ya vijana ‘U-20’, Iddy Salim, aliyefariki dunia kwa ajali ya pikipiki jana Alhamisi,” ilisema sehemu ya taarifa ya klabu hiyo.

Azam FC imeeleza kuwa kifo cha Iddy ni pigo kubwa kwa familia yake, timu ya vijana pamoja na familia nzima ya klabu hiyo, huku ikitoa pole kwa ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huo.

Kwa sasa, mwili wa marehemu Iddy Salim umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala (MRRH) jijini Dar es Salaam, ambako unaendelea kufanyiwa taratibu za mwisho.

Baada ya taratibu hizo kukamilika, mwili wa kipa huyo unatarajiwa kusafirishwa kwenda Tanga, ambako mazishi yatafanyika.

Iddy Salim alikuwa sehemu ya kikosi cha vijana cha Azam FC na alitajwa kama mmoja wa wachezaji waliokuwa wakijenga maisha yao ya soka kupitia mfumo wa vijana wa klabu hiyo.

Kifo chake kimeacha simanzi miongoni mwa wachezaji, makocha na viongozi wa Azam FC, pamoja na familia na marafiki waliomfahamu.

Mungu ailaze roho ya marehemu Iddy Salim mahali pema peponi. AMEN

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
17h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’