APR FC ya Rwanda imefanya comeback kubwa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Aigles du Congo ya DR Congo katika mchezo wa marudiano wa CAF Champions League.
Djibril Ouattara alifungua ukurasa wa mabao dakika ya 32 kabla ya Christian Ishimwe kuongeza la pili dakika ya 58. Ouattara alikamilisha siku yake kwa kufunga bao la tatu dakika ya 75 na kuipa APR FC ushindi wa 3-0.
Ushindi huo umeifanya APR FC kugeuza matokeo ya mchezo wa kwanza ambao Aigles du Congo walishinda kwa bao 1-0. Kwa jumla ya michezo miwili, APR FC imesonga mbele kwa ushindi wa 3-1.
Kwa matokeo hayo, Aigles du Congo wameaga rasmi michuano ya CAF Champions League, huku APR FC ikiendelea na safari yake katika michuano hiyo.