Yanga SC imefanikiwa kusonga mbele katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuichapa Gaborone United ya Botswana kwa mabao 2-1 katika mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Ushindi huo umeifanya Yanga kufuzu kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Botswana kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Yanga iliingia katika mchezo huo ikijua wazi kwamba ilihitaji matokeo mazuri ili kujiweka katika nafasi ya kuendelea na safari yake ya kusaka mafanikio kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika.
Baada ya sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza, presha kubwa ilikuwa kwa upande wa Yanga, hasa kutokana na ukweli kwamba Gaborone United ilikuwa bado na nafasi ya kushtukiza na kuondoka na tiketi ya hatua inayofuata.
Hata hivyo, Wananchi walitumia vyema faida ya kucheza nyumbani na hatimaye kupata ushindi wa mabao 2-1 ambao umeihakikishia timu hiyo tiketi ya kuendelea na mashindano.
Kwa jumla, Yanga imemaliza michezo miwili dhidi ya Gaborone United ikiwa na mabao matatu dhidi ya mawili ya wapinzani wao, matokeo yaliyowatosha kuendelea mbele kwa jumla ya mabao 3-2.
Mafanikio hayo yanaendelea kuonyesha namna Yanga ilivyojijenga katika miaka ya hivi karibuni katika mashindano ya CAF, huku klabu hiyo ikilenga kufanya vizuri zaidi kwenye hatua zinazofuata.
sele mwalimu aongeza historia Mchezo huu pia ulikuwa muhimu kwa upande wa historia ya wachezaji wazawa wa Yanga katika mashindano ya CAF.
Katika miaka ya karibuni, Yanga imekuwa ikipata mabao muhimu kupitia wachezaji mbalimbali katika mchezo wa kwanza wa hatua za mashindano ya CAF.
Katika msimu wa 2022/23, Fiston Mayele alifunga dhidi ya Zalan, huku msimu wa 2023/24 Aziz Ki akiweka jina lake kwenye orodha hiyo baada ya kufunga dhidi ya ASAS ya Djibouti.
Msimu wa 2024/25, Prince Dube alifunga dhidi ya Vital'O, kabla ya Andabwile A kufanya hivyo msimu wa 2025/26 dhidi ya Wiliete Benguela.
Katika msimu huu wa 2026/27, Sele Mwalimu naye alijiunga na orodha hiyo baada ya kufunga dhidi ya Gaborone United katika mchezo wa kwanza.