Ligi Kuu England inaendelea leo kwa mechi mbili zinazotarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wa soka, huku siku ikianza na Coventry City dhidi ya Brighton kabla ya macho yote kuelekea Old Trafford.
Coventry City itakutana na Brighton & Hove Albion kuanzia saa 10:00 jioni, katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Baada ya hapo, muda wa saa 12:30 usiku ni zamu ya mchezo mkubwa wa siku, Manchester United dhidi ya Manchester City katika Manchester Derby.
Derby hii inatarajiwa kuwa na kila kitu; presha, ushindani mkali, mashambulizi, mabao na matukio ya kusisimua. Ni mchezo ambao mara nyingi huja na drama yake ndani ya dakika 90.
Mashabiki wa soka duniani watakuwa wakisubiri kuona nani atatawala Manchester leo, huku United na City zikisaka pointi muhimu katika msimu huu wa Premier League.