International, Normal News, Pyramids, Egypt, Mokwena, CAFCL, Al ahly, Zamalek

Pyramids ya mokwena haishikiki misri, yaandelea kuongoza msimamo

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
1h ago
Pyramids ya mokwena haishikiki misri, yaandelea kuongoza msimamo

Pyramids FC chini ya kocha Rhulani Mokwena imeendelea na mwanzo bora katika Ligi Kuu ya Misri baada ya kuifunga ENPPI mabao 2-1, ushindi uliowafanya kufikisha pointi 15 na kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo baada ya michezo mitano.

Pyramids ililazimika kugeuza matokeo baada ya ENPPI kuanza kwa bao la kuongoza, kabla ya Nasser Maher kusawazisha na Walid El Karti kufunga bao la ushindi dakika ya 87. Ushindi huo umeifanya Pyramids kushinda michezo yote mitano ya ligi hadi sasa.

Katika mashindano ya CAF Champions League, Pyramids pia imeonyesha kiwango kizuri baada ya kuifunga Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza jijini Nairobi, kabla ya kushinda 5-1 katika mchezo wa marudiano Cairo. Matokeo hayo yaliwapa ushindi wa jumla wa mabao 7-1 na kuwawezesha kusonga mbele katika hatua inayofuata.

Mokwena, aliyewahi kufanya kazi katika benchi la ufundi la Mamelodi Sundowns, sasa anaendelea kuiongoza Pyramids katika kampeni yake ya ligi na mashindano ya kimataifa, huku klabu hiyo ikiwa kileleni mwa ligi kwa pointi 15, ikifuatiwa na Zamalek na Al Ahly wenye pointi 13 kila mmoja.

More Stories

EPL kuendelea leo kwa dabi ya London kati ya Brentford dhidi ya Chelsea
EPL kuendelea leo kwa dabi ya London kati ya Brentford dhidi ya Chelsea
2h ago
READ MORE →
Yanga yapambana kuondoa kadi nyekundu ya Aziz Ki kabla ya derby ya simba
Yanga yapambana kuondoa kadi nyekundu ya Aziz Ki kabla ya derby ya simba
5h ago
READ MORE →
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
23h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
23h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
1d ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
1d ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
1d ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
1d ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
1d ago
READ MORE →