Nahodha wa Nottingham Forest, Morgan Gibbs-White, ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa Uingereza kuchukua nafasi ya nyota wa Chelsea, Cole Palmer, ambaye ameondolewa kikosini kufuatia majeraha ya misuli.
Kiungo huyo ambaye alikuwa tayari kuianza likizo ya kifamilia anajiunga na kikosi icho cha "Three Lions" kutokana na kiwango chake bora msimu huu huku akilazimika kuweka kando mipango yake binafsi ili kuungana na wachezaji wenzake wa taifa ilo.
Uingereza itacheza michezo ya hatua ya makundi UEFA Nations League dhidi ya Hispania, Jamhuri ya Czech na Croatia