Raphinha ameteuliwa rasmi kuwa mchezaji anayeshikilia jezi namba 10 ya timu ya taifa ya Brazil, kufuatia kustaafu kwa Neymar Jr. kwenye soka la kimataifa.
Nyota huyo wa Barcelona sasa atavaa namba hiyo yenye historia kubwa katika timu ya taifa ya Brazil, ambayo imewahi kuvaliwa na baadhi ya mastaa wakubwa wa nchi hiyo.
Hatua hiyo inaongeza matarajio kwa Raphinha, ambaye sasa anatarajiwa kuendelea kuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Brazil katika kipindi kijacho.
Raphinha — namba 10 mpya wa Brazil.