Local, Normal News, Taifa stars, Guinea Bissau

Taifa Stars yaangukia pua mbele ya Guinea-Bissau

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
30m ago
Taifa Stars yaangukia pua mbele ya Guinea-Bissau

Taifa Stars ya Tanzania imepoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Guinea-Bissau katika mchezo wa kimataifa, huku wapinzani hao wakitumia vyema nafasi zao na kupata ushindi.

Guinea-Bissau ilipata bao la kwanza dakika ya 33 kupitia Franculino Djú, aliyefunga baada ya kupokea pasi ya mwisho kutoka kwa Beto, na kuifanya timu yake kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Dakika ya 58, Mama Baldé aliongeza bao la pili kwa Guinea-Bissau baada ya kupokea pasi kutoka kwa Dalcio, na kuifanya Tanzania kuwa katika hali ngumu ya kurejea kwenye mchezo.

Hadi dakika 90, Taifa Stars haikuweza kupata bao la kufutia machozi, hivyo mchezo kumalizika kwa Guinea-Bissau kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Taifa Stars sasa itahamia kwenye mchezo wake unaofuata dhidi ya Madagascar, utakaochezwa Septemba 29, 2026 katika uwanja wa Stade d’Honneur, Meknes, Morocco.

More Stories

Manchester City yapatikana na hatia katika mashitaka 114 kati ya 115!
Manchester City yapatikana na hatia katika mashitaka 114 kati ya 115!
2h ago
READ MORE β†’
Cristian Romero nahodha mpya Argentina baada ya Messi
Cristian Romero nahodha mpya Argentina baada ya Messi
4h ago
READ MORE β†’
Stars kuanza na Guinea Bissau kufuzu Afcon 2027 leo
Stars kuanza na Guinea Bissau kufuzu Afcon 2027 leo
5h ago
READ MORE β†’
Raphinha avishwa jezi namba 10 Brazil baada ya Neymar kustaafu kimataifa.
Raphinha avishwa jezi namba 10 Brazil baada ya Neymar kustaafu kimataifa.
8h ago
READ MORE β†’
Sudan mabingwa wa CECAFA U20 baada ya kuifunga tanzania kwa penalti
Sudan mabingwa wa CECAFA U20 baada ya kuifunga tanzania kwa penalti
1d ago
READ MORE β†’
Barcelona yatoa ahadi kwa Tanzania, Wachezaji kuja nchini wakishinda Ubingwa
Barcelona yatoa ahadi kwa Tanzania, Wachezaji kuja nchini wakishinda Ubingwa
1d ago
READ MORE β†’
Makonda avitaka vilabu kumaliza migogoro yao kwa vikao vya ndani
Makonda avitaka vilabu kumaliza migogoro yao kwa vikao vya ndani
1d ago
READ MORE β†’
Serikali yalipa Bilioni 104 kwa ajili ya Afcon 2027
Serikali yalipa Bilioni 104 kwa ajili ya Afcon 2027
1d ago
READ MORE β†’
Gamondi aanza mchakato wa kumpata Nahodha mpya wa Taifa Stars
Gamondi aanza mchakato wa kumpata Nahodha mpya wa Taifa Stars
1d ago
READ MORE β†’