Kuelekea Derby ya Kariakoo ya Oktoba 10, kiungo wa Yanga SC, Duke Abuya, anaingia kwenye mchezo huo akiwa na takwimu zinazomweka wazi kama mmoja wa wachezaji muhimu katika eneo la ulinzi.
Abuya amefanya interceptions 34 katika mechi 5, akicheza jumla ya dakika 429 msimu huu.
Takwimu hizo zinaonyesha mchango wake katika kukata mashambulizi na kuvuruga mipango ya wapinzani, hasa akiwa mbele ya safu ya ulinzi.
Sasa macho yote yanaelekezwa kwenye Derby ya Kariakoo, Abuya ataweza kutumia ubora huo kuisaidia Yanga katika mchezo mkubwa dhidi ya Simba?