Mshambuliaji wa Young Africans (Yanga SC), Selemani Mwalimu (20), ameongezwa kwenye kikosi cha Tanzania U23 kwa ajili ya mchezo wa kesho wa kufuzu AFCON U23 dhidi ya Kenya.
Mwalimu ameungana na Juma Abushiri (18), ambaye naye aliongezwa kwenye kikosi cha U23 baada ya awali kuwa sehemu ya Tanzania U20. Kuongezwa kwa wachezaji hao kunatarajiwa kuongeza chaguo la kocha katika mchezo huo muhimu.
Tanzania inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kazi kubwa baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa mabao 4-1 dhidi ya Kenya. Taifa hilo linahitaji kushinda kwa tofauti ya angalau mabao manne ili kubadilisha matokeo na kusonga mbele kwenye kinyang’anyiro cha kufuzu AFCON U23.
ADVERTISE HERE