Stars U23 yakwama mbele ya Kenya kufuzu Afcon

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2h ago
Stars U23 yakwama mbele ya Kenya kufuzu Afcon

Ndoto ya timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 (Tanzania U-23) kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zimegonga mwamba leo, licha ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya wapinzani wao, Kenya (Emerging Stars), katika mchezo wa marudiano uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali ulitawaliwa na kiwango bora cha mshambuliaji Selemani Mwalimu, aliyefunga mabao mawili, huku bao lingine la Tanzania likiwekwa kimiani na Sheikhan Khamis.

Licha ya jitihada hizo zilizowapa matumaini makubwa mashabiki waliojitokeza uwanjani, ushindi huo haukutosha kuivusha timu hiyo kwenda hatua inayofuata.

Tanzania imeondolewa rasmi mashindanoni kwa jumla ya mabao 5-4 (Aggregate), kufuatia matokeo mabaya ya mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Kenya, ambapo wenyeji walishinda kwa mabao 4-1.

Bao la ugenini walilolipata Kenya leo lilizima kabisa matumaini ya vijana wa Kitanzania kupindua meza.

ADVERTISE HERE

More Stories

Singida Black stars yamaliza kambi Arusha, yaisubiri Dodoma jiji
Singida Black stars yamaliza kambi Arusha, yaisubiri Dodoma jiji
7h ago
READ MORE β†’
Arajiga apewa mechi ya ligi ya mabingwa
Arajiga apewa mechi ya ligi ya mabingwa
8h ago
READ MORE β†’
Kipa wa Benin amtumia ujumbe Messi kabla ya mchezo wa kuaga
Kipa wa Benin amtumia ujumbe Messi kabla ya mchezo wa kuaga
9h ago
READ MORE β†’
Messi kuagwa leo, Argentina ikimkaribisha Benin katika mchezo wa kihistoria
Messi kuagwa leo, Argentina ikimkaribisha Benin katika mchezo wa kihistoria
10h ago
READ MORE β†’
Raphinha hadi 2030, Asaini mkataba mpya ndani ya Barcelona
Raphinha hadi 2030, Asaini mkataba mpya ndani ya Barcelona
10h ago
READ MORE β†’
Olise awasha moto, France yafanya comeback ya 4-1
Olise awasha moto, France yafanya comeback ya 4-1
21h ago
READ MORE β†’
Selemani Mwalimu aongezwa Tanzania U23
Selemani Mwalimu aongezwa Tanzania U23
22h ago
READ MORE β†’
Coastal Union dhidi ya Azam FC yasogezwa.
Coastal Union dhidi ya Azam FC yasogezwa.
22h ago
READ MORE β†’
Kariakoo Derby, Makocha Kupewa Kadi Mbili za Kuomba Review ya FVS
Kariakoo Derby, Makocha Kupewa Kadi Mbili za Kuomba Review ya FVS
1d ago
READ MORE β†’
Rais Mwinyi aridhishwa na kasi ya maandalizi Zanzibar kuelekea Afcon 2027
Rais Mwinyi aridhishwa na kasi ya maandalizi Zanzibar kuelekea Afcon 2027
1d ago
READ MORE β†’