Sarafu yaamua hatima ya Serengeti Boys, yakosa nafasi AFCON U17 2027

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2h ago
Sarafu yaamua hatima ya Serengeti Boys, yakosa nafasi AFCON U17 2027

Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Tanzania, Serengeti Boys, imejikuta katika hali ya kusikitisha baada ya hatima yake katika michuano ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana (AFCON U17) 2027 kuamuliwa kwa kurusha sarafu, licha ya kufanya kampeni iliyoiweka sawa na Somalia kwa matokeo ya uwanjani.

Sare ya Somalia yaweka kila kitu njia panda

Serengeti Boys ilianza mashindano ya kufuzu AFCON U17 2027 ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kenya, Oktoba 10, 2026. Mabao hayo yalifungwa na Dismass Athanas dakika ya 28 na Godfrey Somi dakika ya 57.

Katika mchezo wa pili dhidi ya Somalia, Oktoba 12, 2026, Serengeti Boys ililazimika kuridhika na sare ya bao 1-1. Somalia ilipata bao la mapema kupitia Abdikarin Abdulkadir katika dakika ya kwanza, kabla ya nahodha wa Tanzania, Elick Yusuph, kusawazisha kwa mkwaju wa penalti dakika ya 24.

Kwa matokeo hayo, Tanzania ilikuwa na pointi nne baada ya mechi mbili, huku matumaini ya kusonga mbele yakitegemea matokeo ya mchezo wa mwisho wa Somalia dhidi ya Kenya.

Somalia ilifanikiwa kuifunga Kenya mabao 2-0 katika mchezo wake wa mwisho wa kundi, Jumatano, Oktoba 14, 2026. Ushindi huo uliifanya Somalia kufikisha pointi nne, sawa na Tanzania.

Timu hizo mbili zilikuwa na rekodi zinazofanana: kila moja iliifunga Kenya mabao 2-0 na kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya mpinzani mwingine. Hivyo, zilikuwa sawa kwa pointi, mabao ya kufunga, mabao ya kufungwa na tofauti ya mabao.

Kurusha sarafu kukatumika kutenganisha timu hizo, Somalia wakapata bahati nasibu.

ADVERTISE HERE

More Stories

CAF yawateua waamuzi wanne wa Tanzania kuchezesha mchezo wa CAFCL
CAF yawateua waamuzi wanne wa Tanzania kuchezesha mchezo wa CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Vinicius Junior afungiwa mechi nne, kuukosa mchezo wa El Clasico
Vinicius Junior afungiwa mechi nne, kuukosa mchezo wa El Clasico
5h ago
READ MORE β†’
Villa, PSG, Madrid mambo mazuri katika usiku wa UEFA.
Villa, PSG, Madrid mambo mazuri katika usiku wa UEFA.
11h ago
READ MORE β†’
UEFA Champions League kuendelea leo kwa mechi tisa za kibabe
UEFA Champions League kuendelea leo kwa mechi tisa za kibabe
23h ago
READ MORE β†’
Baleke atamba, Simba haijapata mshambuliaji wa kumzidi
Baleke atamba, Simba haijapata mshambuliaji wa kumzidi
23h ago
READ MORE β†’
Barcelona na Arsenal zatamba Bayern ikiambulia sare katika usiku wa Uefa.
Barcelona na Arsenal zatamba Bayern ikiambulia sare katika usiku wa Uefa.
1d ago
READ MORE β†’
Zanzibar yafungua milango ya vipaji vya vijana kupitia Real madrid foundation
Zanzibar yafungua milango ya vipaji vya vijana kupitia Real madrid foundation
1d ago
READ MORE β†’
Keffe D ahukumiwa kifungo cha miaka 40 hadi maisha mauaji ya Tupac
Keffe D ahukumiwa kifungo cha miaka 40 hadi maisha mauaji ya Tupac
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaichakaza Mashujaa 6-1, Mpanzu atupia mawili.
Simba yaichakaza Mashujaa 6-1, Mpanzu atupia mawili.
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : Simba 6-1 Mashujaa Fc
Highlights : Simba 6-1 Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’