Gwiji wa soka kutoka Ivory Coast, Didier Drogba, mwenye umri wa miaka 48, anatarajiwa kuwasili Tanzania leo Oktoba 16, 2026, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2027.
Tanzania inajiandaa kwa mashindano hayo makubwa ya soka barani Afrika kwa kushirikiana na Kenya na Uganda, ambazo kwa pamoja zitakuwa wenyeji wa AFCON 2027.
Ujio wa Drogba unatajwa kuhusishwa na maandalizi ya mashindano hayo, huku Tanzania ikiendelea kujiweka tayari kwa jukumu lake la kuwa mwenyeji wa moja ya michuano mikubwa zaidi ya soka barani Afrika.
ADVERTISE HERE