Klabu ya USM Alger ya Algeria imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2026/27, baada ya wapinzani wao, The Panthers FC ya Equatorial Guinea, kujiondoa kwenye mashindano kutokana na changamoto za kifedha.
Kujiondoa kwa The Panthers FC kunamaanisha kuwa USM Alger itasonga moja kwa moja hadi hatua ya makundi bila kucheza mechi ya raundi ya pili ya awali, ambayo ilitarajiwa kuwakutanisha timu hizo.
Hatua hiyo imeipa USM Alger nafasi ya kuwa miongoni mwa timu zitakazoshiriki hatua ya makundi ya mashindano hayo ya CAF msimu huu, huku timu nyingine zikiendelea kupambana katika raundi za awali ili kupata nafasi ya kufuzu.
ADVERTISE HERE