Manchester United imelazimika kuondoka na pointi moja baada ya kutoka sare ya mabao 1-1 dhidi ya Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa hii leo.
United ikiwa ugenini ilikuwa ya kwanza kupata bao la uongozi lililofungwa na nyota wake Bryan Mbuemo kabla ya Leeds kurejea mchezo kupitia bao la mshambuliaji wao Calvert Lewin.
Sare hiyo inaiacha Manchester United ikiwa na kazi ya kufanya ili kuimarisha mwendelezo wa matokeo katika michezo inayofuata. Kupoteza nafasi ya kupata pointi tatu kunaweza kuongeza presha kwa kikosi hicho katika mbio za kujiweka kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.
Kwa upande wa Leeds United, kupata pointi dhidi ya Manchester United ni matokeo muhimu katika mchezo wa nyumbani. Hata hivyo, timu zote mbili zitalazimika kuangalia maeneo yanayohitaji maboresho kabla ya kurejea uwanjani katika michezo ijayo ya Ligi Kuu England.