Lamine Yamal ajiandaa kwa hafla ya Ballon dOr 2026

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
2h ago
Lamine Yamal ajiandaa kwa hafla ya Ballon dOr 2026

Nyota wa Barcelona Lamine Yamal ameripotiwa kukodi ndege binafsi kwa ajili ya kusafiri kwenda London kuhudhuria hafla ya utoaji wa tuzo za Ballon dOr itakayofanyika Jumatatu Oktoba 26 2026 katika ukumbi wa London Palladium nchini Uingereza. 

Taarifa hizo zinaeleza kuwa Yamal anatarajia kusafiri akiwa ameambatana na watu wake wa karibu kwa ajili ya kushiriki usiku huo mkubwa unaowakutanisha mastaa wa soka kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Aidha Yamal ameripotiwa kuandaa sherehe maalumu jijini Paris endapo atafanikiwa kushinda tuzo ya Ballon dOr ya mwaka huu. Hatua hiyo imeongeza hamasa miongoni mwa mashabiki wanaosubiri kujua kama kinda huyo wa Barcelona ataweza kutwaa tuzo hiyo yenye heshima kubwa katika soka la dunia.

Hafla ya mwaka huu ina umuhimu wa pekee kwa kuwa ni toleo la 70 la tuzo hizo tangu zilipoanzishwa mwaka 1956. Kwa mara ya kwanza katika historia yake hafla hiyo itafanyika jijini London badala ya Paris.

Yamal ni miongoni mwa wachezaji wanaowania tuzo hiyo baada ya kuendelea kungara akiwa na Barcelona na timu ya taifa ya Hispania. Hata hivyo maandalizi ya sherehe hayamaanishi kuwa tayari ameshinda tuzo hiyo kwani matokeo yatatangazwa rasmi wakati wa hafla.

Mashabiki wa soka sasa wanasubiri Oktoba 26 kwa hamu kubwa ili kujua nani ataibuka mshindi wa tuzo hiyo na kama Yamal ataweza kuandika historia mpya katika umri wake mdogo.

Je Lamine Yamal ataondoka London akiwa na Ballon dOr 2026?

ADVERTISE HERE

More Stories

Diarra aadhibiwa Yanga baada ya kuchelewa kurejea kambini
Diarra aadhibiwa Yanga baada ya kuchelewa kurejea kambini
2h ago
READ MORE β†’
Viingilio vya mchezo wa marudiano wa Simba dhidi ya 15 de Agosto vipo wazi
Viingilio vya mchezo wa marudiano wa Simba dhidi ya 15 de Agosto vipo wazi
2h ago
READ MORE β†’
Ahmed Ally awataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi huku Doumbia akiteuliwa kuwa mgeni rasmi
Ahmed Ally awataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi huku Doumbia akiteuliwa kuwa mgeni rasmi
3h ago
READ MORE β†’
Nasreddine Nabi mlangoni kwa Wydad, mazungumzo yakiendelea
Nasreddine Nabi mlangoni kwa Wydad, mazungumzo yakiendelea
3h ago
READ MORE β†’
UEFA Champions League: Como yaichapa Manchester United, Galatasaray yaibuka dhidi ya Lille
UEFA Champions League: Como yaichapa Manchester United, Galatasaray yaibuka dhidi ya Lille
14h ago
READ MORE β†’
Ni rekodi kwa Yanga, yatinga makundi CAFCL msimu wa nne mfululizo
Ni rekodi kwa Yanga, yatinga makundi CAFCL msimu wa nne mfululizo
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 4-1 CFFA, CAFCL
Highlights : Yanga 4-1 CFFA, CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yafuzu hatua inayofuata CAF Champions League kibabe
Yanga yafuzu hatua inayofuata CAF Champions League kibabe
18h ago
READ MORE β†’
β€œkila mtoto na riziki yake” – Zubeda Sakuru ampongeza Doumbia
β€œkila mtoto na riziki yake” – Zubeda Sakuru ampongeza Doumbia
21h ago
READ MORE β†’
Highlights : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL
Highlights : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL
22h ago
READ MORE β†’