Mashindano ya NBC Premier League yanaendelea leo kwa michezo mitatu inayotarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wa soka nchini. Miongoni mwa mechi zinazotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ni pambano kati ya TRA United na Yanga SC.
TRA United itakuwa mwenyeji wa Yanga SC saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Yanga itaingia uwanjani kusaka matokeo mazuri, huku TRA United ikilenga kutumia vyema faida ya kucheza nyumbani.
Katika mchezo mwingine, JKT Tanzania itakutana na Kagera Sugar saa 12:15 jioni katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam. Baadaye usiku, Namungo FC itakuwa mwenyeji wa Coastal Union saa 2:30 usiku katika Uwanja wa Majaliwa, mkoani Lindi.
Mashabiki wa soka wanatarajia kuona ushindani mkubwa katika michezo hiyo mitatu ya ligi. Je, unazipa nafasi timu gani kupata ushindi leo?