Dladla: Yanga tunadaiwa magoli, soka zuri na ushindani wa hali ya juu

Jairo Mtitu By Jairo Mtitu
•
2h ago
Dladla: Yanga tunadaiwa magoli, soka zuri na ushindani wa hali ya juu

Kaimu kocha wa Yanga SC, Simon Dladla, amesema timu hiyo inalenga kurejea katika ubora wake na kuhakikisha inapata matokeo yanayotarajiwa kuelekea mchezo wao wa NBC Premier League dhidi ya Mashujaa FC, akisisitiza kuwa malengo makubwa ya klabu hiyo ni kumaliza ligi ikiwa nafasi ya kwanza.

Dladla amesema utekelezaji wa mabadiliko ya kimfumo na kimbinu katika mchezo ujao utategemea wachezaji watakaopatikana, lakini amewahakikishia mashabiki kuwa Yanga itashuka uwanjani kucheza soka la kuvutia na kwa ushindani mkubwa.

Ameongeza kuwa benchi la ufundi linatambua changamoto zilizopo na linaendelea kuzifanyia kazi ili kuimarisha timu. Akizungumza na mashabiki wa Yanga, maarufu kama Wananchi, Dladla amekiri kuwa timu hiyo iliwakatisha tamaa katika mchezo uliopita baada ya kushindwa kupata matokeo waliyokuwa wakiyatarajia.

Hata hivyo, amesema wameyabaini mapungufu yao na wamejipanga kufanya kazi kwa bidii ili kurekebisha hali hiyo.

“Kwa Wananchi, tunafahamu kuwa tuliwakatisha tamaa katika mchezo uliopita kwa sababu hatukupata matokeo tuliyokuwa tunayatarajia. Tumeyatambua mapungufu yetu na tutafanya kazi kwa bidii. Tunafahamu kuwa tuna deni kubwa kwenu. Tunadaiwa magoli, tunadaiwa soka zuri na kiwango cha juu cha ushindani kila tunaposhuka uwanjani,” amesema Dladla.

Kwa upande wake, kipa wa Yanga, Aboutwaleeb Mshery, amesema mchezo dhidi ya Mashujaa hautakuwa rahisi kutokana na ushindani ambao timu hiyo imekuwa ikiutoa katika Ligi Kuu.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa wachezaji wa Yanga wamejipanga kupambana kwa juhudi zote ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

“Hautakuwa mchezo rahisi kwa namna ambavyo Mashujaa wanacheza. Ni timu ambayo imekuwa ikitoa ushindani mkubwa kwenye ligi. Nachoweza kuwahakikishia ni kwamba wachezaji tutapambana kwa juhudi zote ili tupate matokeo mazuri,” amesema Mshery.

Kauli za Dladla na Mshery zinaashiria dhamira ya Yanga kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo uliopita na kurejesha imani ya mashabiki wake.

Kwa upande wa benchi la ufundi, kipaumbele ni kuboresha kiwango cha timu, kuongeza ufanisi wa ushambuliaji na kuhakikisha Yanga inaendelea kupambana kufikia malengo yake ya msimu.

ADVERTISE HERE

More Stories

Tanzania yaandika historia, timu nne zote zatinga hatua ya makundi ya CAF kwa mara ya pili mfululizo
Tanzania yaandika historia, timu nne zote zatinga hatua ya makundi ya CAF kwa mara ya pili mfululizo
1h ago
READ MORE →
Usiku wa Ballon d’Or 2026 nani atatwaa tuzo ya dhahabu
Usiku wa Ballon d’Or 2026 nani atatwaa tuzo ya dhahabu
2h ago
READ MORE →
“Matendo yake ni makubwa kuliko umbo lake”: Usiyoyajua kuhusu nyota wa Azam FC, Idd Selemani Nado
“Matendo yake ni makubwa kuliko umbo lake”: Usiyoyajua kuhusu nyota wa Azam FC, Idd Selemani Nado
2h ago
READ MORE →
Kocha Pyramids katika rada za Yanga
Kocha Pyramids katika rada za Yanga
3h ago
READ MORE →
Azam Fc, Singida BS uso kwa uso na wababe 14 makundi CAFCC
Azam Fc, Singida BS uso kwa uso na wababe 14 makundi CAFCC
7h ago
READ MORE →
Simba, Yanga uso kwa uso na miamba wengine 14 makundi CAFCL
Simba, Yanga uso kwa uso na miamba wengine 14 makundi CAFCL
7h ago
READ MORE →
Real Madrid yaiadhibu Barcelona, Mbappe akiendeleza rekodi
Real Madrid yaiadhibu Barcelona, Mbappe akiendeleza rekodi
13h ago
READ MORE →
Simba yatinga hatua ya makundi klabu bingwa kibabe
Simba yatinga hatua ya makundi klabu bingwa kibabe
20h ago
READ MORE →
Highlights : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL
Highlights : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL
21h ago
READ MORE →
Game Kali za leo katika ligi mbalimbali duniani
Game Kali za leo katika ligi mbalimbali duniani
1d ago
READ MORE →