Brighton & Hove Albion imeandika ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu England uliopigwa kwenye dimba la Etihad.
Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Yasin Ayari dakika ya 11, akiipa Brighton uongozi wa mapema na kuifanya Manchester City kushindwa kutumia vyema faida ya kucheza nyumbani.
Matokeo hayo yanaongeza ushindani katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England, huku macho sasa yakielekezwa kwa Arsenal ambao kesho watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Liverpool.
Arsenal watakuwa na nafasi ya kutumia matokeo ya Manchester City kujiongezea nguvu katika mbio za kuwania taji, lakini wanahitaji kwanza kupata matokeo mazuri katika mchezo wao dhidi ya Liverpool.
ADVERTISE HERE